Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Cheka Hija, almaarufu kama Bi. Cheka kutoka Kundi la Mkubwa na Wanawe, linaloongozwa na Said Fella ‘Mkubwa’  nyumba anayoishi msanii huyo mzee mbayo iko maeneo ya Bunju B, nje kidogo ya jiji la Dar iko kwenye hali mbaya ambapo kwa mujibu wake yeye amesema ameshindwa kurekebisha baada ya kusumbuliwa na maradhi toka alipoanguka Oktoba mwaka huu,anasema watu wa mtaani kwake wanavyo mwangilia kwenye Tv na jinsi anavyoishi mtaani kwao ni tofauti kabisa akihojiwa na mtandao wa global publisher alizungumzia haya 




“Ukweli nilikuwa na hali mbaya, afadhali sasa, naongea na kusimama kwani nilikuwa siwezi kutembea, wiki iliyopita alikuja meneja wetu, Yusuf Chambuso na akina Dogo Aslay,Jamani maisha yangu kwa sasa ni magumu kwani siwezi kufanya kazi yoyote na sina msaada na kwenye muziki sijaona faida yoyote labda ya nguo tu, kwamba nilizoea kuvaa madela na kanzu sasa nina suruali,” 

“Kuhusu malipo makubwa kuwahi kupata ni shilingi laki tatu nilizolipwa kwenye shoo ya Fiesta mwaka juzi, hizo ndizo hela kubwa niliyowahi kupata katika muziki.”