Mchezaji Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 sasa ameshinda tuzo nyingine zinazotolewa na shirika kubwa la utangazaji la BBC ambapo amempiku mpinzani Lionel Messi ambaye hajawahi kushinda hata mara moja.
Tuzo hiyo ambayo amepata inajulikana kama BBC Overseas Sports Personality of the Year, mchezaji huyo amekuwa wa nne kushinda tuzo hiyo ambapo wengine ni kama
- Eusebio alishinda tuzo hiyo mwaka 1966
- Pele alishinda tuzo hiyo mwaka 1970
- Brazilian Ronaldo alishinda tuzo hiyo mwaka 2002
Kwenye kuwania tuzo hiyo Cristiano alifanikiwa kumpiku Serena Williams, mcheza masumbwi Floyd Mayweather pia muendesha magari Marc Marquez kwenye kipengele hicho
0 comments:
Post a Comment