Mwanamitindo Flaviana anayewakilisha vizuri Tanzania kwenye mashindo makubwa ya urembo, Novemba mwaka jana yaani 2014 alichumbiwa na mtanzania ambaye bado hatujamjua lakini pale mtakapopata taarifa zake nitakuwekea hapa,

             flaviana-matata

Kupitia kipindi cha XXl kinachorushwa na kituo cha utangazaji cha Clouds Fm alikuwa na haya ya kusema

“Kila kitu kitaendelea kama kilivyo sasa mpaka pale nitakapoona sasa imetosha nifanye mambo mengine, lakini haitabadilisha chochote, itabadilisha status tu ndo inakuwa mrs flani basi.” Alisema kupitia XXL ya Clouds Fm.

Flaviana matata anaingia kwenye list ya mstaa wasiopenda maisha yao ya mapenzi yajulikana sana kama ilivyo kwa Millard Ayo na Ay pia Mwana FA, mchumba wake ambaye ni mtanzania aishie Marekani kwa mujibu wake Flaviana Matata ni nyingine ya kauli yake kuhusu kwanini kuchagua mchumba mtanzania na sio mzungu 

“Utamaduni ni muhimu sana, Kiukweli simzui mtu kuolewa na utamaduni wowote lakini mimi najua nachokihitaji katika maisha yangu, najua hatufanani najua mwingine anataka mzungu mwingine muhindi, lakini mimi cha kwanza kabisa utamaduni ni muhimu sana.”